'Inapomea: Maono ya Wangari Maathai' Filamu ambayo yasimulia maisha na miradi ya ajabu ya Dr Wangari Maathai, mwana-Kenya mashuhuri aliyetunzwa tuzo kuu la Nobel Peace Prize. Tendo lake la upandaji miti lilienea na mwishowe likazambaa kote nchini pamoja na harakati za kuyalinda mazingira, kuzitetea haki za binadamu na kupigania demokrasia. Hadithi hii yaonyesha mapambano yake makali dhidi ukataji misitu, umaskini, udhalimu na ukandamizaji mnamo muda wa miaka thelathini ya maisha yake.
Iwapo una shida za mtandao au ikiwa kwako hupati mkondo video (yaani "streaming"), filamu hii pia yapatikana kwa DVD. Tafadhali uliza maelezo zaidi kupitia takingrootfilm@gmail.com